WONDERS OF HONEY (PROFESSIONAL TALK)
You are what you eat!
Licha ya sifa yake ya kuwa na utamu wa asili usio na madhara hata kwa wagonjwa wa kisukari, asali pia ni tiba ya magonjwa mengi, pia ni kinga ya maradhi yanayosababishwa na bakteria, fangasi na mengine mengi. Asali mbichi ndiyo bora zaidi kuliko iliyopikwa.
ASALI DAWA YA KIFUA KWA WATOTO
Uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo kimoja cha dawa nchini Marekani, (Penn State College of Medicine), ulithibitisha kuwa asali inaweza kutibu magonjwa ya kifua, kikiwemo kikohozi kwa watoto wenye umri kuanzia miaka 2-18. Hivyo kwa mzazi kujenga mazoea ya kuwapa asali wanae ni jambo la busara.
ASALI DAWA YA KISUKARI
Ingawa watu wenye kuugua ugonjwa wa kisukari (type 2) huwa hawaruhusiwi kula vyakula vyenye sukari, lakini wanaweza kula asali kwani ni dawa kwa njia moja ama nyingine, kutokana na kuwa na virutubisho aina ya ‘fructose’ na ‘glucose’ ambavyo vinahusika na udhibiti wa kiwango cha sukari kwenye damu ambavyo havina madhara.Aidha, inaelezwa kuwa ili ini lifanye kazi yake vizuri, linahitaji ‘mafuta’ ya kuendeshea na mafuta ya ini yanapatikana pia kwenye asali, hivyo kwakutumiaasali iliyo bora utaweza kuimarisha utendaji kazi wa ini na hivyo kujiepusha na matatizo [B]ya kiafya [B]ya ini.
ASALI HUONGEZA KINGA YA MWILI
Asali pia inaelezwa kuwa na uwezo wa kuongeza kinga [B]ya mwili. Utafiti uliofanywa katika hospitali kadhaa nchini Israel ulionesha mafanikio hayo kwa aslimia 64 [B]ya wagonjwa waliopewa [B]asali katika utafiti huo na hata asilimia 32 [B]ya wagonjwa wa kansa nao walionesha matumaini mapya [B]ya maisha baada [B]ya[B]kutumia dozi [B]ya [B]asali.
ASALI DAWA YA VIDONDA
Tangu enzi na enzi, asali imekuwa ikitumiwa na mababu zetu kama chanzo cha nishati ya mwili, lakini pia katika utafiti wa hivi karibuni, imegundulika kuwa asali ina ewezo mkubwa sana wa kuponya vidonda vya aina mbalimbali kutokana na viambata vyake kuwa na uwezo wa kukausha maji haraka kwenye kidonda.Aidha, virubisho vingine vilivyomo kwenye asali vina faida kubwa kwa wana michezo kwani huongeza nguvu na wana michezo wengi wamekuwa wakitumia vyakula vitokanavyo na [B]asali au vyenye mchanganyiko wa [B]asali na wameona mafanikio makubwa.
KIJIKO KIMOJA CHA ASALI KINGA YA SIKU NZIMA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, [B]asali ina uwezo wa kutoa kinga dhidi [B]ya vidudu nyemelezi ambavyo husababisha magonjwa mbalimbali mwilini pale mwili unapokuwa hauna kinga. Hivyo kijiko kimoja cha chakula cha [B]asali kikitumiwa kila siku huwa kinga tosha (antioxidants).Kutokana na ubora wa [B]asali, watu wenye ugonjwa wa kisukari aina [B]ya pili (Diabetes 2), wanapotumia [B]asali, utafiti unaonesha kuwa kiwango chao cha sukari kwenye damu hushuka na hivyo kushauriwa [B]kutumia [B]asali kwenye chai na milo yao mingine badala [B]ya sukari nyeupe.
Kwa ujumla [B]asali ina [B]faida nyingi katika mwili wa binadamu, kwani ni chanzo kikubwa cha vitamini na madini. Inaelezwa kuwa [B]asali ni chanzo kizuri cha vitamin B2, B6, madini [B]ya chuma na manganizi (manganese). Anza sasa mazoe ya kula [B]asali, ila hakikisha una pata [B]asali halisi, siyo feki
Comments
Post a Comment